Thursday, January 20, 2011

JIYU IPPON KUMITE NA SENSEI LEFEVRE

VITENDEA KAZI VYA SHINDANO

1. Vibendera vyeupe na vyekundu (5 kwenye pambano).

2. Mbao za alama (7 kwenye pambano).

3. Vifaa vya rekodi (madaftari n.k).

4. Vifaa vya muda.

5. Mikanda myeupe/yabluu na myekundu.

6. Glovu.

7. Filimbi (5 kwenye pambano).

STAFU YA SHINDANO

1. Mratibu wa Shindano:
Atakuwa na jukumu la kusimamia mwenendo mzima wa shindano na
kuhakikisha kila kitu kinaenda kama ilivyopangwa. Majukumu yake
hayato takiwa kuingilia sheria na taratibu za uchezeshaji wa shindano.

2. Daktari wa shindano:
Atasimamia maswala yote yanayohusika na matibabu katika shindano.

3. Timu ya Huduma ya Kwanza (First Aid):
Watatakiwa kuwa tayari kwa tatizo lolote la kiafya linaloweza kujitokeza
katika shindano kwa kusaidiana na Daktari wa shindano.

MAMLAKA YA REFA KATIKA SHINDANO

1. Atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kumaliza pamambano.

2. Atakuwa na mamlaka ya kutoa maamuzi ya jumla.

3. Atakuwa na mamlaka ya kuonya washiriki (kabla, katika na baada ya
mechi) pale itapo mbidi.

4. Atakuwa na uwezo wa kuwaita majaji ili kujadili uamuzi
pale utata utakapo jitokeza.

5. Atakuwa na mamlaka ya kuongeza muda wa pambano pale itapo bidi.

VIGEZO VITUMIKAVYO KUJAJI KATA YA MSHIRIKI/MSHINDANI KATIKA SHINDANO(WKF)

1. Muonekano wa maana ya kata.

2. Uelewa wa mbinu zitumikazo katika kata(BUNKAI).

3. Spidi, mtiririko(RYTHM), fokasi na nguvu.

4. Upumuaji sahihi katika kuitafuta KIME.

5. Uzatiti wa mawazo(CONCENTRATION).

6. Mikao(STANCES) na hatua sahihi.

7. Utumiaji mzuri wa kiuno na tumbo la chini(HARA).

8. Ugumu wa kata.

9. Kutanuka na kusinyaa kwa mwili.

10. Satmina.

11. Uelekeo sahihi wa mbinu.

12. Morali(SPIRIT).

13. Mlio wa shambulizi(KIAI).

14. Vituo(BREAKS).

15. Nidhamu katika matumizi ya nguvu.

16. Kujiamini(CONFIDENCE).

MAMLAKA YA REFA MKUU KATIKA SHINDANO

1. Atakuwa na maamuzi ya mwisho katika shindano.

2. Atawajibika kuhakikisha shindano halikiuki taratibu/kanuni zilizoainishwa.

3. Atakuwa na uwezo wa kuwaita majaji ili kujadili uamuzi
pale utata utakapo jitokeza.

4. Atakuwa na mamlaka ya kuteuwa majaji.

5. Atakuwa na mamlaka ya kubadili majaji pale itapompasa kufanya hivyo.

MAJUKUMU YA MAREFA NA MAJAJI KATIKA MASHINDANO

1. Wanatakiwa kutofungamana na upande wowote katika maamuzi.

2. Wanatakiwa kuwaheshimu washiriki pamoja na maofisa washirika.

3. Maamuzi yao yanapaswa kuwa ya haraka mno na yanayojitosheleza.

4. Wanatakiwa kuzatiti mawazo yao yote katika shindano.

5. Wanatakiwa kuheshimu kanuni za taaluma.

VIGEZO ANAVYOTAKIWA KUWANAVYO REFA WA WKF(WORLD KARATE FEDERATION)

1. Umri
Kumite:Kuanzia miaka 30 na kuendelea.
Kata:Kuanzia miaka 35 na kuendelea.

2. Dani
Kumite:Kuanzia Dani 3 (Sandan) na kuendelea.
Kata:Kuanzia Dani 4 (Yondan) na kuendelea.

3. Majukumu: Kuchezesha:-
(a)Mashindano ya watu wazima(yaani wenye umri wa miaka 18 na kuendelea).
(b)Mashindano ya watu watoto(yaani wenye umri chini ya miaka 18).

4. Muda wa Awamu
Kumite:Miaka 4.
Kata:Miaka 4.

Baada ya kipindi hicho kuisha, refa atapaswa kufanya mtihani wa WKF(Kumite
pamoja na Kata) ili kuendelea kutambuliwa na shirikisho.

5. Mitihani
Kumite:-
(a)Nadharia
(b)Vitendo

Kata:-
(a)Nadharia
(b)Vitendo