Thursday, March 17, 2011

MASTER MANABU MURAKAMI (7 DAN-SKIF) NJIANI KUJA TANZANIA KUIIMARISHA SKI-TZ!

SHIHAN MANABU MURAKAMI KUJA TANZANIA

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SENSEI KOLOWA .P. CHIKOKO
(RAIS WA SKIF TANZANIA) KWA NAMBA ZIFUATAZO) :-

+255-713-464441 au

+255-767-464441 au

+255-688-900080

SENSEI MANABU MURAKAMI AKIPIGA 'DEMO'

SHIHAN MANABU MURAKAMI

Sensei Manabu Murakami anashikilia daraja la saba la mkanda mweusi
( dani saba) kutoka shirikisho la SKIF lililo anzishwa na Kancho
Kanazawa Hirokazu(dani kumi). Sensei Manabu amewahi kutwaa taji
la kombe la dunia la Karate(SKIF) mara mbili ikiwa ni pamoja na
rekodi zifuatazo:-

Mashindano ya tatu ya SKIF, Timu ya Kata na Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya nne ya SKIF, Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya tano ya SKIF, Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya saba ya SKIF, Timu ya Kumite...Mshindi wa kwanza.

Mashindano ya nane ya SKIF, Kumite...Mshindi wa kwanza.

Murakami Sensei alizaliwa mwezi wa kumi, mnamo mwaka 1966 Kyushu,
kusini mwa Japan. Alianza kujihusisha na Karate akiwa na umri wa
miaka tisa chini yausimamizi wa Sensei Maruo aliyekuwa mwalimu
wa JKA. Kacho Kanazawa alipo unda shirikisho la SKIF mnamo mwaka
1978, bila kusita Sensei Manabu Murakami akajiunga na SKIF na
kujitoa JKA. Baada ya kumaliza masomo yake katika chuo kikuu cha
Takushoku,Sensei Murakami akaamua kujiunga na kozi ya ualimu ya
SKIF ambayo aliihitimu baada ya miaka miwili. Baada ya hapo Sensei
Murakami akaamua kufundisha katikadojo kuu ya SKIF (Japan) ambako
yuko mpaka leo hii.

Sensei Manabu Murakami anashauri wanafunzi wafurahie mafunzo ya
Karate,iwe ni moja ya burudani sambamba na kuwa taaluma. Kwa namna
hiyo ana amini mwanafunzi ataweza kufika mbali sana kitaaluma
kutokana na ufundishaji mzuri na mvuto atakaoendelea kuupata
katika sanaa hii ya mapigano.

SKI-TZ YAWALETEA SHIHAN MANABU MURAKAMI (7DAN) KUTOKA DOJO KUU(JAPAN)





SENSEI MANABU MURAKAMI (7 DAN) NJIANI KUJA TANZANIA

'MASTER OF MASTERS' KANCHO H . KANAZAWA( 10 DAN)

Kancho H.Kanazawa ni moja kati ya walimu wakubwa wa sanaa ya mapigano
walio hai. Ni moja kati ya walimu wachache waliofundishwa na O'Sensei
Funakoshi Gichin katika enzi za uhai wake.

Kanazawa Sensei alizaliwa mwaka 1931 huko Japani, na kama makarateka
walio wengi wa enzi hizo, alianza sanaa ya mapigano kwa kujifunza Judo.
Wakati alipokuwa akisoma katika chuo kikuu cha Takushoku, ndipo
alipoanza mafunzo ya Karate chini ya M.Nakayama aliyekuwa mwalimu mkuu
wa Japan Karate Association (JKA).

Huko Japani H.Kanazawa alichukua umaarufu mnamo mwaka 1957 alipokuwa
akishiriki mashindano ya taifa(All Japan Karate Championship) na kuibuka
mshindi katika mechi zote akiwa amevunjika mkono na kukiuka ushauri wa
daktari. Mama yake alikuwa moja ya washabiki kwenye jukwaa na inasemekana
kwasababu hiyo, Kanazawa hakutaka 'kumuangusha'. Kilikuwa ni kitu cha
ajabu kwasababu watu aliokabiliana nao walikuwa si wakuingilika hata
unapokuwa na silaha.

Baada ya kumaliza programu ya ualimu ya JKA, Kanazawa akapangiwa kwenda
kufundisha Hawaii, baada ya miaka mitano, mnamo mwaka 1966, akapelekwa
Uingereza ambako alipatadani ya sita ya Shotokan Karate kutoka kwa walimU
wakuu wa JKA.

Uungwana, ucheshi na unyenyekevu wake uliwashangaza wengi kutokana na
mamlaka pamoja na heshima aliyokuwa nayo. Mnamo mwaka 1967 aliteuliwa
kuwa mwalimu mkuu wa JKA katika bara la ulaya.

Hatahivyo, mnamo mwaka 1977, Kanazawa akiwa na dani saba alilazimishwa
kuondoka JKA kutokana na sababu za kiofisi. Watu wengi wakajua kwamba
ulikuwa ni mwisho wa malengo na safari yake katika sanaa ya mapigano.
Ndipo alipoanzisha Shotokan Karate International Federation (SKIF).
Shirikisho lenye zaidi ya wanafunzi 2,000,000 hivi leo, Tanzania ikiwa
ni moja ya nchi wanachama chini ya uongozi wa Sensei Kolowa.P.Chikoko.
Hiyo idadi 'inawafunga mdomo' watu wengi ambao hawakumtakia mema.

Ukiachiliambali mafanikio yake kishirikisho, lakini pia Kancho Kanazawa
ameandika vitabu vingi vya Karate na muongozo wa kiroho kwa ujumla ambavyo vimenunuliwa kwa wingi mno dunia nzima. Kanazawa kama Funakoshi na Nakayama
ni mtu anayeendelea 'kuumiza kichwa' katika kuiboresha sanaa hii tukufu ya
mapigano.


SENSEI MANABU, KANCHO KANAZAWA NA SENSEI CHIKOKO(TANZANIA)





KANCHO KANAZAWA(10 DAN) AKITOA MAELEZO KWA SENSEI CHIKOKO(3 DAN)


KANCHO KANAZAWA



















SENSEI MANABU MURAKAMI KUJA TANZANIA