KARATE

MAANA YA KARATE

Neno karate ni muunganiko wa maneno mawili ya kijapani, yaani ‘kara’ na ‘te’.
1. ‘kara’ inamaanisha au kuelezea
(a)Pasipo silaha.
(b)Fikra iliyo huru(tupu) na yenye kuakisi
                                                                       mazingira yanayoizunguka bila
                                                                       kubugudhiwa.
2. ’te’  inamaanisha mikono.
      Hivyo basi karate kama neno moja ni ‘mikono mitupu’ ikiwa na maana ya   kujihami pasipo
     matumizi ya silaha.
     Kimsingi karate ni sanaa inayoendelezwa kupitia mila ,desturi na tamaduni mbalimbali ikiwa
     na malengo yafuatayo:-
(a) Kumuwezesha msanii wake kuweza kujihami katika mazingira hatarishi bila kujali
     umri, nguvu, umbo au jinsia aliyonayo.
(b)Kumpa karateka(msanii wa karate) afya njema iliyo imara.
(c)Na kubwa kuliko yote, kupigania mwenendo sahihi wa tabia. Hili ndilo lengo kuu la karate.

                       HISTORIA YA KARATE KWA UFUPI

Kutoka kwenye mchoro ufuatao :-




                                                     NAMNA  KARATE  ILIVYO STAWI

Takriban miaka mia sita iliyopita, mfalme Sho-Hashi wa Okinawa alianzisha sera iliyopiga
marufuku  umiliki wa silaha katika visiwa vya Okinawa.
Mnamo mwaka 1609, silaha zote zilitaifishwa na serikali ya Okinawa. Hiyo ikapelekea watu
wengi  wa Okinawa kujifunza mbinu za kujihami pasipo kutumia silaha, ndipo karate ilipo melea.
Hivi leo karate inaendelea kustawi  kutokana na faida mbalimbali ambazo watu wanatarajia
kuzichuma kutoka kwenye sanaa hiyo ikiwa ni pamoja na muongozo wa kiroho au tabia,
sababu za kiuchumi,mbinu za kujihami n.k.

                                              BAADHI YA FAIDA ZA  KARATE
•KUPIGANIA MWENENDO SAHIHI WA TABIA
Lengo kuu  la karate si ushindi dhidi ya mpinzani au jambo fulani bali ni ushindi
dhidi ya nafsi yako mwenyewe. Hii ndio karate-do. Neno ‘do’ lina maana ya ‘njia’.
Sote tunajua kwamba hakuna mtu kati yetu aliye mkamilifu hivyo basi ni vema
kila mmoja wetu akajitahidi kupunguza madhaifu yake katika safari ya maisha
yake. Hii ndio njia ya karate yaani ‘ karate-do’.
Madhaifu yanayoelezwa hapa ni kama hasira kali, uzinzi, ulevi, aibu iliyokithiri
au kutokujiamini, woga, uvivu, tamaa, husuda, chuki, kujisikia, dharau, majungu n.k.
Ni vema ikaeleweka kwamba sanaa haimjengi mtu bali mtu ndiye
huijenga sanaa ikiwa na maana ya kuifanya karate kuwa sanaa bora na muhimu
katika maisha yetu tofauti kabisa na ambavyo imekuwa ikichukuliwa.
Lakini kamwe karate haitoweza kumsaidia mtu kitabia mpaka pale atakapo pata
mafunzo kutoka kwa mwalimu ambaye ni msomi na mtaalamu wa sanaa hiyo.
Wataalamu na wasomi wa karate wapo wachache mno na walimu wengi si wataalamu
hivyo ni vema kuwa makini mara mtu atafutapo shule ya kujifunza kwasababu ni
vigumu mno kupima utaalamu na elimu ya mwalimu.

•UWEZO WA KUJIHAMI PASIPO KUHITAJI SILAHA
Kama ndege, wanyama na mimea mbalimbali ina namna au mbinu za kujihami
kwanini  asiwe binadamu ?!.

Karate inamuwezesha  karateka  kuweza kujihami katika mazingira hatarishi
pasipo kujali umri, jinsia,nguvu au umbo alilonalo. Itagharimu nguvu ndogo sana
pamoja na ustadi sahihi wa mbinu ya karate katika kuimudu hali ya hatari.

•NIDHAMU NA KUJITAMBUA KATIKA MAZINGIRA MBALIMBALI
Karateka ni  lazima muda wote awe mwenye nidhamu, aitambue nafsi yake
pamoja na mazingira yanayomzunguka. Hii itamuwezesha kutimiza wajibu wake pale
atakapo hitajika kufanya hivyo. Lakini pia karateka kama mtu yoyote atakuwa
na marafiki wenye tabia mbalimbali hivyo kuna wakati atatakiwa kuheshimu
maamuzi na mitazamo yao pindi watakapo kuwa pamoja. Hii kwenye karate
tunaita  ‘ roho yenye muafaka ‘.

•AFYA NJEMA ILIYO IMARA
Karate inamsaidia karateka katika kuimarisha afya yake kupitia mazoezi na taratibu
mbalimbali zilizopo mafunzoni. Waweza kuitumia karate katika kupunguza  uzito
wa mwili, kujenga misuli yenye nguvu, kujenga mifupa na viungo imara n.k.

•MTU YEYOTE ANAWEZA KUJIFUNZA KARATE
Tofauti na sanaa nyingi za mapigano, karate haimbagui mtu katika mafunzo yake.
Pasipo kujali jinsia, umri, nguvu au umbo; mtu  yeyote anaweza kuanza mafunzo
ya karate hata kama ana umri wa miaka hamsini(50) na kuendelea alimradi
atakuwa akifundishwa na mwalimu mtaalamu na msomi wa karate ambaye ataweza
kutofautisha mafunzo kulingana na umri, jinsia, nguvu na umbo la mwanafunzi.

        BAADHI YA MATATIZO YANAYOIKUMBA KARATE  YA TANZANIA

•UTAALAMU WA WALIMU WA KARATE
Walimu wengi hapa nchini hawana taaluma ya kutosha  kuhusiana na karate, hiyo inapelekea
kutoa mafunzo yasiyo sahihi na hatimaye kutoa picha potofu juu ya sanaa hii.
Hii ni pamoja na jamii kudhani kwamba karate ni swala la ngumi na mateke tu au ni sanaa
inayoweza kufundishwa kwa  jinsia fulani au umri fulani tu. Wengine hugubikwa na
hofu ya kuvunjika viungo, kupiga watu hovyo, kuwa jambazi, kupoteza maisha n.k.
Karate ni sanaa nzuri sana kama ikifundishwa kwa usahihi lakini ni sanaa mbaya mno
na hatari kama itafundishwa na mwalimu asiye na taaluma ya kutosha kuhusu karate.


•HALI NGUMU YA KIUCHUMI
Mitihani ya kimataifa ya madaraja ya karate ni gharama mno ukilinganisha na hali ya
kiuchumi ya makarateka wengi wa Tanzania.
Gharama ya kila mtihani wa kimataifa wa madaraja ya mkanda mweusi si chini ya dola 100 za
kimarekani.  Tanzania ina walimu wachache mno wenye mamlaka ya kutahini japo daraja la
kwanza la mkanda mweusi, hiyo inapelekea watu kufikiria  aidha kumleta mwalimu kutoka nje
ya nchi ikiwa ni pamoja na kugharamia tiketi ya ndege(kuja na kurudi), mahali
atakapo fikia, usafiri n.k au mtahiniwa kwenda nje ya nchi ili kutahiniwa.

•MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA KARATE
Ijapokuwa karate haibugudhiwi sana na ukubwa wa eneo la mafunzo tofauti na sanaa au
michezo mingine lakini karate ni lazima ifundishwe kwenye sakafu nyororo  isiyo na muinuko.
Vilevile mahali pakufundishia  karate ni vema pakafunikwa au kuzungushiwa uzio ili kuondoa
mazingira ya wanafunzi kubugudhiwa na watu wataoamua kutazama mafunzo ya karate.
Tanzania ina shule chache mno za karate zinazo zingatia viwango vya kimataifa .

•UTAPELI
Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa mstari wa mbele  na hata kujitangaza  kwenye
      vyombo vya habari kwamba ni waalimu wakubwa wa sanaa ya karate pasipo na utaalamu
wa sanaa hiyo.  Wengine huangalia video za sanaa mbalimbali za mapigano na kuzitumia
video hizo kama nyenzo za kufundishia, wakati wengine hutoa historia za uongo kuhusu
hatua mbalimbali walizopitia katika kujifunza sanaa hii ikiwa ni pamoja na kutaja majina
ya walimu maarufu wa karate duniani.
Mara nyingi watu wa namna hii hutumia kujiamini kwao ili kumshawishi mwanafunzi
kwamba ni walimu wakubwa wa sanaa hii ya mapigano. Hivyo basi ni vema  mtu ambaye
anataka kujifunza sanaa hii akafanya utafiti wa kutosha ijapokuwa ni ngumu ili kupata
mwalimu  mtaalamu na msomi atakayeweza kutoa mafunzo sahihi.

•ELIMU DUNI/POTOFU KATIKA JAMII YA KITANZANIA KUHUSIANA NA KARATE
Karate imekuwa ikichukuliwa kama sanaa hatari na isiyofaa kundishwa katika jamii
mbalimbali.  Mitazamo kama hii ambayo ni ya kisiasa huwanyima haki watu
wanaoipenda sanaa hii na walio tayari kujifunza kwa moyo mmoja. Nimeshuhudia
vijana wakitimuliwa mahali fulani ili wasiendelee kujifunza karate kwa hofu za
kisiasa kwamba huenda walikuwa wakijifunza  na kumilikiwa na chama fulani cha
siasa kwa sababu za kiulinzi.
Lakini pia kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiogopa kujifunza sanaa hii kwa
hofu ya umri, jinsia, kuvunja viungo, kupoteza maisha n.k.
Kuna wakati ni haki yao kufikiria hivyo kutokana na picha wanayoipata kutoka kwenye
shule mbalimbali zinazoendeshwa na walimu wasio na taaluma ya kutosha
kuhusiana na sanaa hii. Walimu hawa wasio wasomi wa sanaa hutoa mafunzo
potofu ambayo hutoa picha mbaya katika jamii na kusababisha baadhi ya wanafunzi
kukimbia mafunzo.

•UHABA WA MAFUNZO YA KARATE  KATIKA MASHULE NA VYUO MBALIMBALI
Japan iliweza kuiendeleza vizuri karate kutokana na sera za kuipeleka katika vyuo,
mashule na taasisi mbalimbali za elimu na utamaduni. Baadhi ya walimu wakuu
wa mashule mbalimbali nchini Tanzania wamekuwa wagumu kushawishika katika
kuifanya karate kama moja ya michezo mashuleni. Hii ingeweza kuwasaidia sana
wanafunzi  kinidhamu,kiafya , kitabia na kimtazamo.

TOFAUTI BAINA YA KUNG FU NA KARATE
Ni kawaida kwa watu wengi wasio jifunza sanaa za mapigano na hata baadhi wanafunzi wa sanaa
hizi kujiuliza juu ya tofauti baina ya karate na kung-fu.
(Kwa wale watakaotaka kujua historia ya kuzaliwa kwa karate kwa ufupi, naomba warejee kwenye
makala zangu za januari 2010)

Kimsingi karate sambamba na staili nyingi za sanaa ya mapigano imezaliwa kutoka kwenye
kungu-fu. Karate imeundwa na kuwekwa katika mfumo ambao mtu yeyote ataweza kujifunza
na kuwa mkufunzi pasipo kujali umri, jinsia, nguvu au umbo la msanii. Tofauti na karate,
kung-fu kwa ujumla haipo kwenye mfumo ambao kila mtu ataweza kujifunza kiurahisi. Kuna
staili nyingi za kung-fu ambazo hutegemea sana umri wa mtu anayetaka kujifunza, nguvu yake,
ulaini wa viungo, wepesi, jinsia n.k.

Ijapokuwa mtu anayetaka kujifunza kung-fu anaweza akatafuta staili inayo endana na umbile
lake au jinsia aliyonayo lakini anaweza kushindwa kujifunza staili iliyompendeza na
bado atakuwa katika wakati mgumu kwasababu bado mifumo ya kung-fu iko mingi mno na hiyo
ni pamoja na ugumu wa kupata mwalimu anayefundisha mfumo atakaoutaka. Karate ina staili chache
mno ukilinganisha na kung-fu, na hii inarahisha upatikanaji wa staili ya msanii popote aendapo.

Hivyo tunaona ni jinsi gani ambavyo kung-fu ina kaubaguzi fulani tofauti na staili nyingi
za karate. Lakini hii si kusema kwamba karate ni rahisi na kung-fu ni ngumu au kinyume chake,la, kiufundi hakuna staili ya sanaa za mapigano iliyo bora au rahisi kuliko nyingine.
Inategemea na yule msanii wa ile sanaa kwamba anaiwakilisha vipi sanaa yake mbele ya hadhira.

Msanii wa karate anaweza kuionyesha sanaa yake mbele ya hadhira na kuzikonga nyoyo za
watazamaji kuliko msanii wa kung-fu, au msanii wa kung-fu kuwapendeza watu kuliko wa karate.
Hii yote itategemea na msanii. Hiyo ni kusema kwamba hakuna staili mbovu bali kuna wasanii wabovu. Na tena hakuna mwanafunzi mbovu ila kuna walimu wabovu. Tukimuangalia mwanafunzi tunapata taswira kwamba mwalimu atakuwaje pasipo kujali kipaji cha mwanafunzi.

Kitaalam, mbinu nyingi za kung-fu zipo katika mifumo ya mduara(circular) wakati mbinu nyingi
za karate zipo katika mifumo minyoofu(linear).

Katika karate, kwa madaraja ya awali, viwango hutofautishwa na rangi za mikanda mpaka pale
karateka atakapofikia mkanda mweusi tayari kuendelea na madaraja ya mkanda mweusi. Wasanii wa
kung-fu kwa kawaida huwa hawana mifumo ya rangi za mikanda n.k. Kuna wakati hutofautisha
viwango vya wasanii kwa kutumia rangi za mavazi ya mazoezi.

Staili nyingi za karate huchezwa peku (kwa watakaotaka kujua sababu naomba warejee kwenye makala yangu ya kwanza ya mwezi huu), wakati saili nyingi za kung-fu huchezwa na viatu.

Katika karate, kwa kawaida matumizi ya silaha hufundishwa katika madaraja ya juu(mpaka msanii atakapoweza
kujimudu vyema pasipo utegemezi wa silaha) tofauti na kung-fu ambapo wasanii wengi hutumia
muda wao wote wa mafunzo kujifunza au kufundishwa namna ya kuzimudu baadhi ya silaha za mapigano.

Nimejitahidi kuelezea tofauti baina ya karate na kung-fu kwa kadri ya uwezo wangu, ni matumaini
yangu itawawia rahisi kujaribu kutafautisha baina ya hizi staili mbili za mapigano. Tofauti ya
haraka-haraka ni kwamba maranyingi(na si wakati wote) karateka huwa kwenye mavazi meupe,peku na kiwango hutegemea mkanda aliouvaa wakati wa kung-fu huweza kuwa kwenye mavazi yenye rangi mbalimbali kama orenji, njano, bluu, nyeusi n.k, akiwa amevaa viatu na vitambaa vya mavazi yao huwa laini.

MSANII WA KARATE(SENSEI GEORGE BEST).

WASANII WA KUNG-FU.


      BAADHI YA STAILI ZA KARATE
•Shotokan  (Prof. Funakoshi  Gichin)
•Shotokai  (Sensei Shigeru Egami na Sensei Hironishi)-Wanafunzi  wa  F.Gichin
•Goju-Ryu (Sensei Kanryo Higaonna)- Mwanafunzi mwenza wa  F.Gichin
•Shito-Ryu (Sensei Mabuni Kenwa)-Mwanafunzi mwenza wa  F.Gichin
•Wado-Ryu (Sensei Otsuka Hironori)- Mwanafunzi  wa   F. Gichin
•Kyokushinkai ( Sensei Masutatsu Oyama)-Mwanafunzi  wa   F. Gichin

WAASISI WA STAILI MBALIMBALI ZA KARATE
Profesa Gichin Funakoshi

(SHOTOKAN)


Sensei Mabuni Kenwa
(SHITO RYU)




Sensei Higaonna Kanryo
(GOJU RYU)


Sensei Otsuka Hironori

(WADO RYU)


Sensei Masutatsu Oyama
(KYOKUSHINKAI)


Sensei Shigeru Egami na Sensei Hironishi

(SHOTOKAI)


MISEMO YA KUKUMBUKWA KUTOKA KWA
MWALIMU MASHUHURI WA KARATE

Kama kioo kiwezacho kutoa taswira safi pasipo bugudha, au bonde lililo kimya liwezalo kutoa mwangwi,ndivyo mtu anayejifunza karate-do apaswavyo kuwa mbali na fikra za uovu au ubinafsi na kuwa mwenye fikra safi yenye kujitambua, inayoakisi kile inacho kipokea kikamilifu.
Master Gichin Funakoshi
"Karate-do Kyohan"


Karate-Do si swala la kumjuza mtu mbinu za kujihami peke yake bali ni pamoja
na kumudu namna ya kuwa mtu mwenye tabia nzuri na mnyenyekevu katika
jamii .
Master Gichin Funakoshi
"My Way of Life"



SHULE YA SHOTOKAN KARATE ILIYOPO MWENGE (2008)


Sensei Kolowa .P. Chikoko(mbele) akitoa mafunzo,mstari wa kwanza kutoka kushoto ni Majaliwa na katikati ni Caesar(Mhariri wa blog hii)

INDIA 2009



Kushoto ni Caesar akiwa na Sensei Subramanian K.V


INDIA(Bangalore), 2009


Caesar wa pili kutoka kulia (waliosimama), wa tatu ni Sensei Subramanian.

18 comments:

  1. Nawezaje kufika chuo cha mafunzo kareti dar es salaam

    ReplyDelete
  2. Napenda haya mafunzo ya karate

    Mi nipo kahama shinyanga

    Nitakuwa pamoja nawe ktk makala hii

    Na Mungu akubariki

    ReplyDelete
  3. Chuo kipo maeneo gan mm nip dar

    ReplyDelete
  4. Nataka kitabu cha shotokani kareti

    ReplyDelete
  5. Chuo kipo dar sehem gani nahitaji kujiunga na mafunzo9

    ReplyDelete
  6. Nahitaji kujifunza naomba nipe maelekezo nini nifanye

    ReplyDelete
  7. Nataka kuanza mafunzo ya karate naomba maelekezo.

    ReplyDelete
  8. Hakuna kitu kizuri na ninachokipenda Kama hiki ebu fanyeni mpango walau kila mkoa kuwe na kituo hata Kama ni kidogo, kwani binafsi makosa mwalimu hivyo naishia kujifunza mtandaoni Jambo ambalo ni gumu kwa kiasi kikubwa

    ReplyDelete
  9. Nipe bei ya mafunzo Mimi nije chuo Na inapatikana wapi hicho chuo Mimi nipo Arusha

    ReplyDelete
  10. Napenda kujifunza lakini sijui pakujifunzia naomba anayefahamu tuwasiliane kupitia 0715049634

    ReplyDelete
  11. Myahudi napendaaa sanaa kujifunzaa mchezoo huu 0717812423

    ReplyDelete
  12. Naomba yeyote anaeweza niunganishaa anichek 0623723074 plse

    ReplyDelete