KANCHO KANAZAWA

Kancho H.Kanazawa(10TH DAN) ni moja kati ya walimu wakubwa wa sanaa ya mapigano
walio hai. Ni moja kati ya walimu wachache waliofundishwa na O'Sensei
Funakoshi Gichin katika enzi za uhai wake.

Kanazawa Sensei alizaliwa mwaka 1931 huko Japani, na kama makarateka
walio wengi wa enzi hizo, alianza sanaa ya mapigano kwa kujifunza Judo.
Wakati alipokuwa akisoma katika chuo kikuu cha Takushoku, ndipo
alipoanza mafunzo ya Karate chini ya M.Nakayama aliyekuwa mwalimu mkuu
wa Japan Karate Association (JKA).

Huko Japani H.Kanazawa alichukua umaarufu mnamo mwaka 1957 alipokuwa
akishiriki mashindano ya taifa(All Japan Karate Championship) na kuibuka
mshindi katika mechi zote akiwa amevunjika mkono na kukiuka ushauri wa
daktari. Mama yake alikuwa moja ya washabiki kwenye jukwaa na inasemekana
kwasababu hiyo, Kanazawa hakutaka 'kumuangusha'. Kilikuwa ni kitu cha
ajabu kwasababu watu aliokabiliana nao walikuwa si wakuingilika hata
unapokuwa na silaha.

Baada ya kumaliza programu ya ualimu ya JKA, Kanazawa akapangiwa kwenda
kufundisha Hawaii, baada ya miaka mitano, mnamo mwaka 1966, akapelekwa
Uingereza ambako alipatadani ya sita ya Shotokan Karate kutoka kwa walimu
wakuu wa JKA.

Uungwana, ucheshi na unyenyekevu wake uliwashangaza wengi kutokana na
mamlaka pamoja na heshima aliyokuwa nayo. Mnamo mwaka 1967 aliteuliwa
kuwa mwalimu mkuu wa JKA katika bara la ulaya.

Hatahivyo, mnamo mwaka 1977, Kanazawa akiwa na dani saba alilazimishwa
kuondoka JKA kutokana na sababu za kiofisi. Watu wengi wakajua kwamba
ulikuwa ni mwisho wa malengo na safari yake katika sanaa ya mapigano.
Ndipo alipoanzisha Shotokan Karate International Federation (SKIF).
Shirikisho lenye zaidi ya wanafunzi 2,000,000 hivi leo, Tanzania ikiwa
ni moja ya nchi wanachama chini ya uongozi wa Sensei Kolowa.P.Chikoko.
Hiyo idadi 'inawafunga mdomo' watu wengi ambao hawakumtakia mema.

Ukiachiliambali mafanikio yake kishirikisho, lakini pia Kancho Kanazawa
ameandika vitabu vingi vya Karate na muongozo wa kiroho kwa ujumla ambavyo vimenunuliwa kwa wingi mno dunia nzima. Kanazawa kama Funakoshi na Nakayama
ni mtu anayeendelea 'kuumiza kichwa' katika kuiboresha sanaa hii tukufu ya
mapigano.


SENSEI MANABU, KANCHO KANAZAWA NA SENSEI CHIKOKO(TANZANIA)





KANCHO KANAZAWA(10 DAN) AKITOA MAELEZO KWA SENSEI CHIKOKO(3 DAN)


KANCHO KANAZAWA



















No comments:

Post a Comment